Wednesday, September 26, 2012

http://sphotos-c.ak.fbcdn.net/hphotos-ak-ash4/c120.0.403.403/p403x403/430392_359758620714368_681508041_n.jpg

ISHARA ZA MWANAUME AMBAYE HANA NIA AU HATAKI KUWA NA WEWE KATIKA MAHUSIANO YA KUDUMU (NDOA) NA WAKATI KIPINDI HICHOHICHO ANAKUTAMKIA NENO “NAKUPENDA”..


1.HAPIGI SIMU, BALI HUTUMIA SMS

Je, Kijana Huyu Aliyekwamb
ia Anakupenda Huwa Anawasiliana Nawe Kwa Njia Ya Ujumbe Mfupi Kuliko Anavyokupigia? Kama Utaona Hivyo, Basi Una Kila Sababu Ya Kuanza Kuitilia Shaka Nia Ya Kijana Huyu Wa Kiume, Kwani Kwa Hakika Hana Nia Yoyote Ya Dhati Ya Kuendelea Kuwa Nawe.

Kijana Wa Kiume Anapompenda Msichana, Hutamani Muda Wote Kuisikia Sauti Yake. Anapokuwa Anasisitiza Kutumika Kwa Ujumbe Mfupi Maana Yake Hana Haja Sana Ya Kusikia Sauti Yako. Naam, Ujumbe Mfupi Wa Maneno Si Njia Rahisi Sana Ya Kuwasiliana, Lakini Zaidi Ni Njia Rahisi Zaidi Ya Kuepuka Mawasiliano Na Kutoa Majibu Mafupi Kwa Mtu Ambaye Usingependa Kuwasiliana Naye.

2.ANA SABABU ZA KUCHELEWA

Unaweza Kubaini Katika Mikutano Yako Miwili-Mitatu Na Kijana Aliyekwambia Anakupenda, Kwamba Si Mtu Wa Kujali Wala Kutunza Muda. Naam, Yawezekana Katika Mara Mnazokutana, Mara Nyingi Zaidi Anachelewa Kuliko Anavyowahi. Unaweza Kudhani Kuwa Kijana Huyu Ana Mambo Mengi, Au Si Mzuri Katika Upangiliaji Wake Wa Muda, Lakini Kwa Hakika Hupaswi Kumtafutia Visingizio Hata Kama Unampenda, Kwani Kuna Uwezekano Mkubwa Kuwa Kijana Huyu Hana Mpango Na Wewe.

Kijana Wa Kiume Akikupenda Na Kupenda Kuendelea Kuwa Nawe, Lazima Tu Atakuwa Na Msukumo Wa Kutaka Kukutana Na Wewe Na Hatapenda Kukuudhi Kwa Kuchelewa. Mtu Huyu Hata Kama Atakuwa Amebanwa Vipi Kazini Ni Rahisi Sana Kutafuta Muda Wa Kukutana Na Wewe. Kinyume Chake Atakuwa Ni Mtu Wa Visingizio Vya Kuchelewa Na Wakati Mwingine Kutofika Kabisa Katika Eneo La Miadi – Hususan Kama Ameshakupata.

3.ANAWASILIANA NA MPENZI WA ZAMANI

Mwanamume Asiye Na Mpango Wa Kuendelea Kuwa Nawe Anapokuwa Amekutongoza Na Pengine Mmekutana Mara Moja Au Mbili, Atakutaarifu Kwa Kuendelea Kuwasiliana Na Mpenzi Wake Wa Zamani.

Kwa Hakika, Hakuna Jambo Ambalo Humsahaulisha Mwanamume Mpenzi Wa Zamani Kama Kumpata Mpenzi Mpya Anayempenda Kwa Dhati. Iwapo Ataendelea Kuwasiliana Na Kuzungumza Na Mpenzi Wake Wa Zamani, Hiyo Ni Ishara Kuwa Hajamalizana Na Mpenzi Wake Huyo Wa Zamani Na Pengine Bado Anatarajia Kurudiana Naye. Lakini La Muhimu Zaidi Ni Kwamba, Mwanamuke Huyu Hakupendi Kama Unavyodhani Na Wala Hajawa Tayari Kuwa Nawe Kama Mpenzi Au Mchumba.

4.HAKUTAMBULISHI KWA MARAFIKI

Mwanamume Akikupenda, Hususan Vijana Katika Zama Hizi, Lazima Tu Atakutambulisha Kwa Marafiki Zake, Maana Atakuwa Anajisikia Fahari Kwa Kufanya Hivyo, Hususan Kama Anahisi Wewe Ni Mwanamke Maridadi.

Kwa Hulka, Lazima Tu Kijana Wa Kiume Atataka Kujionesha Kwa Watu Anapokuwa Na Kimwana Maridadi Na Anayempenda Kwa Dhati. Usipoona Dalili Zozote Za Jambo Hili, Basi Chukulia Tu Kuwa Kijana Huyu Wa Kiume Hajakupenda Kama Unavyodhani.

5.HUEPUKA WATU KUWAONA PAMOJA

Mwanamume Asiye Na Mpango Wa Kuendelea Kuwa Nawe Katika Uhusiano, Hujitahidi Kuepuka Watu Kuwaona Pamoja. Ni Kweli Kuwa Si Vijana Wote Wa Kiume Wanaopenda Mapenzi Ya Maonesho Ya Kushikana Mikono Wanapotembea, Lakini Kama Ameridhika Nawe Lazima Tu Kwa Kiasi Fulani Atataka Umma Ujue.

Kwa Hakika, Kijana Wa Kiume Anapokuwa Amempenda Msichana Kwa Dhati, Hujikuta Akifanya Hata Mambo Ambayo Zamani Alikuwa Hadhani Kuwa Anaweza Kuyafanya, Ikiwa Ni Pamoja Na Kuonesha Mapenzi Hadharani, Japo Kwa Idhara Ndogo Ndogo. Kwa Tamaduni Za Magharibi Ni Kawaida Kumbusu Mpenzi Hadharani Au Kumzungushia Mkono Kiuononi, Au Kumshika Mkono, Au Kumbusu. Lakini Afrika Hata Kutoka Naye Nje Mkizungumza Huwafanya Watu Washuku Jambo. Kama Hukuliona Hilo Kwa Mpenzi Wako, Basi Chukulia Tu Kuwa Unapoteza Muda.

6.HAZUNGUMZII MIPANGO YA BAADAYE

Unapokuwa Unazungumza Na Mwanamume Ambaye Ana Mpango Wa Kuwa Nawe Katika Kipindi Chake Cha Maisha Yaliyobaki, Lazima Tu Utambaini Akiingiza Mambo Yanayohusiana Na Maisha Ya Baadaye Mkiwa Pamoja. Kwa Hakika, Utambaini Mwanamume Huyu Akitumia Nafsi Ya Kwanza Wingi Tena Katika Muda Wa Baadaye, Yaani Akizungumza Mambo Ambayo Atafanya Na Wewe Miaka Ijayo.

Iwapo Atazungumzia Klabu Fulani Aliyoiona Karibuni Lakini Akawa Hagusii Kuwa Mtakwenda Huko Siku Moja – Tena Mbaya Zaidi Akawa Anasema Kuwa Huwa Anakwenda Pale Mara Kwa Mara, Basi Tambua Kuwa Hauko Katika Mipango Yake Ya Baadaye.

7.HAKUNA MATENDO YA MAHABA

Mwanamume Asiye Na Mpango Wowote Na Wewe Si Aghalabu Kukufanyia Jambo Ambalo Utaliona La Kimapenzi Au La Kimahaba, Hususan Anapokuwa Amefanikiwa Kufanya Mapenzi Na Wewe. Ukiona Hivi, Shtuka Mapema Na Anza Kuangalia Ustaarabu Mwingine.

Haina Maana Kuwa Asipokununulia Maua Basi Hana Mpango Nawe, Lakini Angalau Mara Moja Moja Akufanyie Jambo Au Angalau Atoe Kauli Ambayo Itakusisimua Na Kukufanya Ujione Wa Thamani Na Wa Pekee Machoni Pake.

8.MIPANGO UNAPANGA WEWE

Iwapo Utabaini Kuwa Asilimia 80 Ya Mambo Mnayofanya Pamoja Unayaanzisha Wewe, Basi Una Kila Sababu Ya Kuutilia Shaka Mustakabali Wa Uhusiano Wenu.

Kama Ilivyobainishwa Awali, Mwanamume Akikupenda Atataka Mwe Pamoja Muda Mwingi, Lakini Kama Utabaini Kuwa Mipango Mingi Unaanzisha Wewe Na Unazungumza Naye Kwenye Simu Ijumaa Na Mnamaliza Bila Mwanamume Huyu Kuonesha Dalili Za Kutaka Kuwa Nawe Wikiendi, Japo Kwa Kinywaji, Basi Chukulia Kuwa Mwanamume Huyu Hana Nia Yoyote Ya Kuwa Nawe Kwa Muda Mrefu Zaidi.

9.HANA MPANGO NA WATU WAKO

Mwanamume Anayekupenda Atajishughulisha Na Mambo Yanayohusiana Na Watu Wako Wa Karibu, Hususan Ndugu, Jamaa Na Marafiki Zako. Iwpao Utabaini Kuwa Mwanamume Huyu Haulizi Swali Lolote Kuhusiana Na Familia Yako Au Marafiki Zako, Basi Tambua Kuwa Hana Mpango Wowote Wa Maana Na Wewe. Kumbuka Mwanamume Akikupenda Hujaribu Kuwafahamu Na Kuwapenda Watu Wako, Maana Amependa Boga Na Sheria Ni Kwamba Lazima Upende Na Ua Lake.

10.HAKUMBUKI LOLOTE LA MAANA

Ni Wazi Kuwa Hujakaa Sana Na Mwanamume Huyu, Lakini Angalau Kuna Mambo Muhimu Umefanya Naye Ambayo Anapaswa Kuyakumbuka. Kama Hawezi Kukumbuka Tarehe Muhimu Za Uhusiano Wenu, Mathalani Tarehe Mliyokutana Mara Ya Kwanza, Au Siku Mliyofanya Mapenzi, Basi Yamkini Mwanamume Huyu Hana Mpango Wowote Wa Dhati Wa Kuendelea Kuwa Nawe.

USIPOTEZE MUDA

Hakuna Mtu Mwenye Lengo La Kukuvunja Moyo, Lakini Ujumbe Ulio Dhahiri Ni Kwamba, Kama Unafikiria Uhusiano Wa Kudumu Na Mtu Kisha Akawa Anaonesha Ishara Zilizobainishwa Hapa, Basi Tambua Tu Kuwa Huyo Si Wako Na Atakupotezea Muda Wako Bure. Wala Usijaribu Kumlazimisha, Maana Mambo Ya Kulazimisha Huwa Hayadumu.

Ni Muhimu Sana Kuhakikisha Kuwa Mtu Unayetaka Kujenga Naye Uhusiano Wa Kudumu Anakupenda Kwa Dhati. Wala Haipendezi Kumng’ang’ania Mtu Ambaye Mapenzi Yake Kwako Ni Nusu Nusu. Hakikisha Kuwa Mtu Unayempenda Na Unayetaka Kuwa Naye Ni Yule Ambaye Amekuzimikia Na Atamani Sana Kuwa Nawe. Mtu Huyu Utampata, Hususan Kama Wewe Mwenyewe Utaweka Jitihada Za Makusudi Na Kujiweka Katika Hali Ya Kupendwa Na Kupendeka.
— with Prissy Kipingu and 42 others.

Hakuna Ambaye Ni Msafi Kwa Asilimia Mia Moja

Katika Maisha Kuna Kitu Kuridhika. Unapokuwa Na Mtu Ambaye Anakupa Kila Aina Ya Furaha Maishani Mwako Bila Kuonesha Tabia Zozote Zinazokutia Mashaka Juu Ya Penzi Lake, Huyo Mpende, Mheshimu Na Muamini, Hata Kama Kuna Uwezekano Wa Yeye Kuwa Anaficha Makucha Yake Na Kuyachomoa Pale Anapokuwa Mbali Na Wewe, Kwa Sababu Huna Uhakika Na Hujawahi Kumuona, Chukulia Kwamba Yeye Ni Msafi Kisha Yaache Maisha Yenu Yaendelee Kuwepo.

Nasema Hivyo Kwa Sababu, Tukianza Kuchunguzana Hakuna Ambaye Ni Msafi Kwa Asilimia Mia Moja. Kila Mtu Anajiamini Mwenyewe

Lakini Huwezi Kuiamini Nafsi Ya Mwenzako Kwa Asilimia Zote.

IJUE SIFA ZA "MWANAUME ATAKAYE KUOA" NA "MWANAUME ANAYEKUCHEZEA"


ATAKAYEKUOA SIFA ZAKE NI KAMA IFUATAVYO...

1. ANABADILIKA


Mwanaume Ambaye Ana Malengo Ya Kuoa Hubadilika Kitabia. Muda Mwingi Hutaka Kuonekana Mtu Mzima Mwenye Sifa Nzuri. Hatakuwa Mtu Wa Kulewa Kupita Kiasi Na Kutapanya Mali Na Wanawake Wengine. Tabia Zake Mbaya Za Zamani Ataziacha

Kisa Cha Mabadiliko Hayo Kinatajwa Na Wataalamu Wa Masuala Ya Ndoa Kuwa Ni Pamoja Na Kumshawishi Mwanamke Aliyemchagua Aitikie Mwito Wa Kuwa Pamoja Katika Maisha. Lakini Pia Ni Kuwapa Kielelezo Chema Ndungu Au Wazazi Wake Wamuunge Mkono Katika Harakati Zake Za Kuoa.

2. ATAONGEZA JITIHADA ZA KUJITEGEMEA

Mara Nyingi Wanaume Walio Makini Na Tayari Kufunga Ndoa, Wanahitaji Kuwa Na Kipato Cha Kutosha Kuweza Kuwahudumia Wake Zao Na Familia Ambazo Watakuwa Nazo Hapo Baadaye Hivyo Wanajitahidi Kutafuta Njia Za Kupandisha Hali Yao Kiuchumi.

Kama Ni Muajriwa Anaweza Akaanza Kutafuta Miradi Mingine Nje Ya Kazi Yake Ili Imsaidie Kuongeza Kipato Cha Kujikimu Na Hali Ya Maisha. Kama Alikuwa Anaishi Na Wazazi Atapanga Chumba Na Ataanza Kujitemea.

3. ANAGUNDUA KWAMBA ANAHITAJI KUITWA BABA

Njia Nyingine Ya Kugundua Mwanaume Aliye Tayari Kwa Ndoa Ni Pale Unapotembea Naye Barabarani, Anawafurahia Watoto Mnaokutana Nao Njiani Na Mara Kwa Mara Ataonekana Kukueleza Jinsi Atakavyowafanyia Watoto Wake Mara Baada Ya Kuwapata Hapo Baadaye.

Mwanaume Huyo Pia Huwa Na Tabia Ya Kufurahia Maisha Ya Ndoa Ya Watu Wengine Yaani Anapomuona Mke Na Mume Wakiwa Na Mtoto Wao Basi Hutamani Sana Mngekuwa Nyinyi. Mnapotoka Hukuita Mke Wake!

4. NI RAFIKI LAKINI NI MUME KAMILI

Mwanaume Anayetaka Kuoa Anakuwa Ni Rafiki Yako Tu Kwa Sababu Hamjafunga Ndoa, Lakini Matendo Anayokufanyia Hayana Tofauti Na Yale Ya Mtu Kwa Mkewe. Kwa Mfano Kupanga Mipango Ya Baadaye Ya Maisha Yenu, Kukutambulisha Kwa Ndugu Na Rafiki Zake. Huwa Na Hamu Ya Kutaka Kujua Matatizo Yako Na Kukusaidia Na Wakati Mwingine Kukushirikisha Katika Matatizo Yanayomkabili.

Mara Nyingi Huwa Makini Sana Kutambua Mabadiliko Ya Mapenzi Na Hutoa Uhuru Na Kukumilikisha Vitu Vyake Kwa Mfano Kukupa Funguo Za Chumba Au Nyumba Yake. Hupenda Kutoa Misaada Ya Kumwendeleza Mpenzi Wake Kimaisha, Kama Kumsomesha Au Kumtafutia Kazi.

5. HUFURAHIA UKARIBU

Mwanaume Aliyetayari Kuoa Hupenda Kuwa Karibu Na Mpenzi Wake Na Asilimia Kubwa Ya Mazungumzo Yake Atayaelekeza Katika Maisha Si Ngono. Atajitoa Kusaidia Ndugu Wa Mke Kila Linapokuja Tatizo. Na Atalalamika Anapotengwa Na Familia Ya Mchumba Wake.

SIFA ZA MWANAUME ANAYEKUCHEZEA

1. ANAKWEPA MAZUNGUMZO YA NDOA

Haonyeshi Kufurahi Unapoanzisha Mazungumzo Kuhusu Suala La Kufunga Ndoa Na Wala Hapendi Kuzungumzia Hilo. Wakati Mwingine Hata Kukutambulisha Kwa Ndugu Zake Au Rafiki Inakuwa Shida.

2. ANAGHARAMIA ANASA KULIKO MAMBO MUHIMU

Anakuwa Ni Mtu Wa Kukununulia Mapambo Ya Gharama Na Vitu Vyote Vya Anasa, Lakini Hana Mawazo Ya Kuzungumzia Maisha Yenu Ya Baadaye Wala Kukununulia Vitu Ambavyo Vitakuwa Na Manufaa Katika Maisha Ya Mbeleni. Haangalii Masuala Ya Elimu Wala Kukutafutia Mtaji Au Kazi.

3. HAJALI MACHOZI YAKO

Unaweza Kugundua Ni Jinsi Gani Hana Mpango Mzuri Na Maisha Yako, Kwani Hata Anapokuudhi Anakuwa Hajali Wala Haumizwi Na Machozi Yako, Ni Busara Kuwa Makini Kwa Sababu Huyo Atakuwa Ni Mtu Wa Kukupa Maumivu Wakati Wote.

4. HAJITOKEZI HADHARANI

Mwanaume Ambaye Malengo Yake Ni Kukuchezea Huwa Hataki Mapenzi Yenu Yajulikane Hadharani Atakuwa Mtu Wa Kutaka Mambo Yaende Kwa Siri. Hajitambulishi Kwa Rafiki Wala Kwa Ndugu Zako. Hatoi Nafasi Ya Wewe Kumtembelea Nyumbani Kwake.

SIKU NJEMA NA NINAWATAKIA KAZI NJEMA...

Yafurahie Matatizo Yako Ya Sasa Kwani Ndo Mafanikio Yako Ya Kesho, Uwatafutao Leo Kesho Watakutafuta, Na Wakuchukiao Sasa Muda Ukifika Watakupenda.! Waliosema Hawakupendi Chunga Sana Kauli Zao Maana Watazikana Kauli Zao! Pia Wakupao Moyo Sasa Usiwasahau Maana Ndio Chanzo Cha Mafanikio Yako. Enjoy Your Life! Good Day…

KWA NINI KILA SIKU UNAKIMBIWA NA WANAWAKE ??


Wewe Mwanaume Unayesoma Hapa, Jiulize; Huwa Unadumu Na Mwenzi Wako? Unaachwa Au Kukimbiwa Baada Ya Muda Mfupi? Kama Jibu Ni Ndiyo, Hapa Utapata Tiba. Sikia Nikuambie, Wapo Wengi Ambao Kila Wakianzisha Uhusiano, Siku Mbili Tatu, Mwanamke Anamkimbia.

Anampenda Sana, Anamfanyia Kila Kitu Ambacho Yeye Anaamini Kinakidhi Kwa Mwanamke Wake, Lakini Baada Ya

Muda Mfupi Sana, Anaachwa! Anabaki Kujiuliza Maswali Yasiyo Na Majibu. Rafiki Yangu, Lazima Ujue Kwamba Pamoja Na Kuwa Mapenzi Hayana Kanuni Za Moja Kwa Moja, Zipo Ndogo Ndogo Ambazo Zikifuatwa, Mateso Kwako Yatakuwa Ni Kitendawili.

Huwezi Kukimbiwa Na Wanawake Bila Sababu Za Msingi, Lazima Kuna Kitu Kinachosababisha Uachwe. Hapo Sasa Hakuna Sababu Moja, Wewe Ukiachwa Kwa Sababu Hii, Mwingine Atakimbiwa Kwa Sababu Ile. Katika Darasa Hili, Ukijifunza Kwa Umakini Utaweza Kujua Kasoro Yako Ilipokuwa Na Kufanya Mabadiliko Ili ‘Usiachike’ Tena!

Wanaume Huwa Wanawalaumu Zaidi Wanawake Kutokana Na Sababu Za Hapa Na Pale Zinazosababisha Kuachana Kwao. Lakini Wengine Hutoswa Bila Kuelezwa Sababu Za Msingi, Akibaki Na Maswali Mengi Lakini Mwisho Hupata Msichana Mwingine Kabla Ya Kuachana Naye Tena Bila Kujua Sababu Halisi.Wakati Mwingine Sababu Zenyewe Huwa Za Maana Lakini Zingine Mh! Ni Aibu Kuzitaja Hadharani. Hata Hivyo, Kuna Wengine Huamua Kuachana Na Wapenzi Wao Kwa Makosa Ambayo Wao Hudhani Ni Makosa Kumbe Wao Ndiyo Wanaokosea! Hebu Tuone…
UKOJE?Kama Una Tatizo La Kuachana Na Wapenzi Kila Wakati, Kipegele Hiki Kinakuhusu! Anza Kuangalia Tabia Zako Upya. Unaishije Na Mpenzi Wako, Jirani Zako Na Watu Wanaokuzunguka? Unatumiaje Ulimi Wako? Wasichana Wengi Wanapenda Wanaume Wachangamfu Na Wacheshi Wakiamini Kwa Namna Moja Ama Nyingine, Ni Burudani Kwao Lakini Huwa Hawapendi Kabisa Uwachangamkie Wengine Kupita Kiasi.Wanaume Wengi Hupingana Na Hili Lakini Utafiti Unaonyesha Kwamba, Asilimia 70 Ya Wanaume Wanaowachangamkia Sana Wanawake, Mwisho Wake Hufanya Nao Mapenzi Kama Siyo Kuingia Katika Uhusiano Moja Kwa Moja. Usibishe, Tafiti Uone!Kama Una Tabia Hii, Hata Kama Unaamini Kwamba Uchangamfu Wako Siyo Wa Nia Mbaya Kwa Wanawake, Achana Nao Maana Unamkwaza Mpenzi Wako Bila Kujua. Wakati Mwingine Anaweza Kuonyesha Wivu Lakini Mwingine Hawezi Kusema, Hivyo Hubaki Akiumia Moyoni Mwake Lakini Akichoka Huamua Kuachana Na Wewe Hata Kama Anakupenda Akihofia Kuwa Katika Penzi La Kuchangia. Angalia Vizuri Tabia Zako Katika Kipengele Hiki.

MWANAMKE MATUNZO!

Hapa Jamani Inabidi Tuambiane Ukweli, Tena Bila Kufichana! Kuna Baadhi Ya Wanaume Ni Wabahili Sana, Yaani Kutoa Fedha Kwa Wapenzi Wao Wanaona Shida Sana. Visingizio Vya Kwamba Wao Siyo Mabuzi Ndiyo Vimewajaa Akilini Mwao.Utawasikia Wakisema; “Mimi Siyo Buzi Bwana, Demu Wangu Halafu Nimlipie? Haiwezekani!” Achana Na Hizo Fikra Ndugu Yangu. Unatakiwa Utoe Matunzo Kwa Mpenzi Wako. Siyo Lazima Mpaka Akuambie! Ni Jukumu Lako Kufahamu Aina Za Vipodozi Anavyotumia.Mnunulie Bila Kukuambia, Mpelekee, Kuwa Mbunifu, Ukiona Nywele Zake Zinaanza Kufumuka, Mpe Fedha Ya Saluni, Tena Ikiwezekana Mchagulie Mtindo Uupendao. Leo Asuke Rasta Za Kimasai, Baada Ya Wiki Kadhaa Unambadilishia Mtindo Mwingine.Jiulize Kama Wewe Ndiye Mpenzi Wake Halafu Unakataa Kumpa Matunzo, Unataka Nani Amhudumie? Hivi Ulivyokutana Naye Akiwa Mzuri, Anapendeza Unadhani Ni Nani Aliyekuwa Anamhudumia?Nakuhakikishia Ndugu Yangu, Kama Huna Utamaduni Wa Kutoa Matunzo Kwa Mpenzi Wako Tarajia Kukimbiwa! Kwa Maneno Mengine Ni Kwamba, Kama Hutoi Matunzo Kwa Mpenzi Wako Ni Kama Umemruhusu Awe Katika Uhusiano Na Mwanaume Mwingine Ambaye Atatoa Matunzo.Ni Wajibu Wako Kumnunulia Mavazi, Manukato Na Hata Fedha Za Matumizi Yake Binafsi. Tatizo Hili Huwakumba Hata Wanandoa, Hawataki Kuwahudumia Wake Zao, Wakidai Kwamba Wameshaoa! Usimpompendezesha Atapendeza? Na Asipovutia Unadhani Nini Kitafuata Kama Siyo Kutafuta Mwanaume Mwingine Nje? Upo Tayari Kusalitiwa?

Inawezekana Unashangaa Kwa Nini Wanawake Wanakukimbia Kila Siku, Kumbe Kuna Sehemu Fulani Huwa Unakosea Bila Kujua. Hapa Ndipo Kwenye Dawa. Ndiyo Sehemu Pekee Utakayoujua Ukweli Na Kuchukua Hatua.
Katika Sehemu Ya Kwanza, Wiki Iliyopita Nilianza Kwa Kuelezea Tabia Mbili; Moja Ikiwa Kujiangalia Upya Tabia Zako Na Pili Ni Kumpa Matunzo Mwenzi Wako.
Lazima Wanaume Mfahamu Kwamba Hata Gari Linapoharibika Huhitajika Kupelekwa Gereji Kwa Kufanyiwa Ukarabati. Vivyo Hivyo Hata Mwanamke Anahitajika Kupewa Matunzo Ili Aendelee Kuwa Bora Na Anayekuvutia.
Ukweli Ni Kwamba, Wanaume Wengi Hukwepa Kutoa Matunzo Ya Karibu Kwa Wapenzi Wao Wakidai Wanachunwa! Nani Amekudanganya Ndugu Yangu? Kumtunza Mpenzi Wako Siyo Kuchunwa!
Mpendezeshe Apendeze, Usipofanya Hivyo Wewe Unataka Nani Akutunzie? Kama Una Tabia Hii Badilika Haraka, Maana Wanawake Wa Sasa Wapo Makini Kuangalia Wanaume Ambao Wanatambua Wajibu Wao.
Kuna Mwingine Huwa Hatoi Fedha Mpaka Siku Atakayolala Na Mpenzi Wake, Hiyo Ni Mbaya Zaidi Maana Hisia Za Kwamba Umemnunua Huanzia Hapo.
Najaribu Kuwaweka Sawa Na Kuwakumbusha Kwamba Mwanamke Anahitaji Matunzo Na Kama Ukishindwa Kumtunza Utakuwa Unampa Mwanya Wa Kutafuta Mwanaume Mwingine. Hapo Ndiyo Mwanzo Wa Usaliti.

UKOROFI, UKALI SI DAWA!

Watu Wanatambua Kwamba Mwanaume Ndiye Kichwa Cha Nyumba, Lakini Hilo Lisiwe Kigezo Cha Wewe Kuwa Mkorofi Na Mjeuri Hata Kwa Mambo Mengine Yasiyo Ya Msingi.
Mwanamke Anahitaji Mwanaume Mwenye Msimamo, Asiyeyumbishwa, Lakini Pia Anatamani Sana Kusikilizwa Mawazo Yake. Mwanamke Anahitaji Kuliwazwa Na Mpenzi Wake.
Ukali Kupindukia Hupunguza Mapenzi Na Hujenga Woga Na Hofu. Wakati Mwingine Hushindwa Kukushirikisha Katika Mawazo Yake Mazuri Ambayo Yangeweza Kujenga Kwa Kuhofia Ukali Wako.
Ni Vizuri Kuwa Makini Katika Hili, Huna Sababu Ya Kuwa Mkali Kwa Mpenzi Wako. Mwanamke Ni Mtu Wa Kuelewa, Kama Kuna Mahali Amekosea, Zungumza Naye Taratibu Huku Upendo Wa Kweli, Utii Na Utu Ukionekana Usoni Mwako Na Hata Kinywani Mwako.

UMAPEPE

Kuna Baadhi Ya Wanaume Wana Tabia Ya Umapepe, Nikisema Hivyo Naamini Naeleweka. Hili Ni Tatizo Lingine Wasilopenda Wanawake. Siyo Wanawake Pekee Bali Hakuna Mtu Atakayejisikia Vizuri Mpenzi Wake Kuwa Na Tabia Ya Umalaya. Kila Mmoja Anapenda Kuwa Na Penzi La Peke Yake Na Siyo La Kuchangia!
Ikiwa Una Tabia Za Kupenda Kubadilisha Wanawake Kila Wakati, Tarajia Kuachana Nao Kila Siku. Lazima Mwanaume Uwe Na Staha, Mapenzi Ya Kweli Na Mtulivu Kwa Mwenzio.
Naomba Nieleweke Kitu Kimoja Hapa, Wakati Mwingine Hata Tabia Zako Za Ajabu Ajabu, Zinamkosesha Raha Mpenzi Wako Na Fikra Za Kuachana Na Wewe Zikizidi Kuusumbua Ubongo Wake.
Epuka Tabia Ya Kusifia Wanawake Wengine Vijiweni Au Ukiwa Na Mpenzi Wako Katika Matembezi. Unapaswa Kujiheshimu. Heshima Unayoionesha Kwa Mpenzi Wako Ni Kithibitisho Tosha Kwamba Unampenda Na Kuheshimu Uwepo Wake.

MPE KIPAUMBELE

Mwanamke Mwenye Mapenzi Ya Kweli Kwako, Lazima Atatamani Kujua Mambo Mengi Kuhusu Wewe, Lakini Kubwa Zaidi Ni Uwazi Kuhusu Maisha Yake Pamoja Na Kutoa Ushauri Kwako Pale Utakapohitajika.
Anapenda Kuona Ukimpa Nafasi Ya Kwanza Katika Maisha Yako, Uwe Wazi Kwa Kila Kitu Kinachoendelea Katika Maisha Yako. Nafasi Ya Kwanza Ninayoizungumzia Hapa Ni Pamoja Na Kuwa Naye Karibu Na Kumpa Taarifa Za Mipango Yako Ijayo, Lakini Katika Hilo, Pia, Mwanamke Anapenda Kuona Unaitambua Thamani Yake Na Kuyashika Maisha Yake Ipasavyo.
Mwanamke Akiona Hapewi Kipaumbele Na Mpenzi Wake, Hupoteza Imani Ya Kuwa Na Mwanaume Huyo. Kama Una Tabia Hizi, Ndugu Yangu Achana Nazo, Vinginevyo Kila Siku Utaishia Kubadilisha Wanawake Kama Nguo.

jana na leo

Yafurahie Matatizo Yako Ya Sasa Kwani Ndo Mafanikio Yako Ya Kesho, Uwatafutao Leo Kesho Watakutafuta, Na Wakuchukiao Sasa Muda Ukifika Watakupenda.! Waliosema Hawakupendi Chunga Sana Kauli Zao Maana Watazikana Kauli Zao! Pia Wakupao Moyo Sasa Usiwasahau Maana Ndio Chanzo Cha Mafanikio Yako. Enjoy Your Life! Good Day… — with Decran Hau